27 Oktoba 2025 - 21:26
Iran na Oman zimekuwa zikisaidiana daima katika nyakati za mivutano ya eneo

Hamad bin Faisal Al-Busaidi alielezea furaha yake kwa ziara yake nchini Iran na kukutana na Rais Pezeshkian, akisema kuwa uhusiano wa Iran na Oman ni wa kipekee, wa kihistoria, wa kina na wa ukweli, usio na mashaka. yoyote.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (a.s) -ABNA- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dkt. Massoud Pezeshkian, amesema kuwa uhusiano wa muda mrefu na wa kirafiki kati ya Iran na Oman umejengwa juu ya misingi ya udugu, heshima ya pande zote na nia njema, akibainisha kuwa nchi hizo mbili zimekuwa zikisaidiana daima katika nyakati zote za mivutano ya kikanda.

Akizungumza leo Jumatatu (5 Aban 1404 H.Sh, sawa na 27 Oktoba 2025) katika mkutano wake na Hamad bin Faisal bin Said Al-Busaidi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Oman, Dkt. Pezeshkian alitambua na kusifu jukumu muhimu la Oman katika medani za kikanda, hususan katika juhudi za upatanishi na uenyekiti wa mazungumzo kati ya Tehran na Washington. Alisema hatua hizo zinaonyesha busara, hekima na dhamira ya amani ya viongozi wa Oman.

Aidha, Rais Pezeshkian alisifu msimamo wa wazi wa Oman wa kuiunga mkono Gaza na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni, akisema:

“Msimamo huu wa kibinadamu na Kiislamu wa Oman una thamani kubwa. Kama mataifa yote ya Kiislamu yangesimama kwa umoja namna hii, tusingeshuhudia matukio ya huzuni na mateso yanayoendelea huko Gaza.”

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Rais wa Iran alisisitiza umuhimu wa umoja wa Umma wa Kiislamu, akisema kuwa kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu na maelekezo ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w), Waislamu wote ni ndugu na mkono mmoja, na endapo watazingatia misingi hiyo, Uislamu utakuwa nguvu kubwa duniani inayolinda maslahi na usalama wa mataifa yote ya Kiislamu.

Dkt. Pezeshkian alionyesha matumaini kwamba ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Oman itaimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, akisisitiza kuwa Iran iko tayari kupanua mahusiano yake na Oman katika nyanja zote - kielimu, kiuchumi, kitamaduni, kijamii na kisiasa.

Kwa upande wake, Hamad bin Faisal Al-Busaidi alielezea furaha yake kwa ziara hiyo nchini Iran na kukutana na Rais Pezeshkian, akisema kuwa uhusiano wa Iran na Oman ni wa kipekee, wa kihistoria, wa kina na wa ukweli, usio na mashaka yoyote.

Akimkumbusha Rais Pezeshkian kuhusu ziara yake ya miezi mitano iliyopita mjini Muscat na makubaliano yaliyofikiwa, Waziri wa Oman alisema kuwa hatua hizo zinaashiria mwelekeo mzuri wa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Alisisitiza kuwa Oman itaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuimarisha na kuendeleza uhusiano wa kirafiki na wa kindugu uliopo kati ya nchi hizo mbili kwa nguvu mpya na dhamira thabiti.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha